Idadi
ya waliofariki kutokana na shambulizi la Kanisa Mombasa Kenya March 23
2014 imefikia sita ambapo wote hao vifo vyao vimetokana na majereha ya
risasi huku wengine tisa waliokua wakipata matibabu hospitali
wakiruhusiwa kwenda nyumbani.Mkuu wa Polisi Kenya amesema bado
hawajafutilia mbali kwamba lilikua shambulio la kigaidi ambapo kwa
mujibu wa Erick Ponda ambae ni mwandishi wa habari wa DW Mombasa
alieongea mpaka March 24 2014 jioni watu 59 walikua wamekamatwa na Polisi kwenye msako wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo.
Wakati
huohuo, mtoto ambae bado kichwani kwake kuna risasi aliyopigwa kwenye
shambulio hilo amepelekwa kwenye hospitali ya binafsi kwa matibabu
maalum kwa sababu anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake.
Mama
mzazi wa mtoto huyu alifariki kwenye hili shambulio hivyo kwa sasa mtoto
yuko na ndugu wa mama yake ambae namkariri akisema ‘haendelei vizuri
manake amekua akinisumbua hawezi kulala, ana maumivu makali sana
kichwani kutokana na hiyo risasi ndani ya kichwa’
Viongozi
wa kidini wakiongozwa na Askofu Julius Atsango wamewataka wenzao wa dini
ya kiislamu kuisaidia serikali kuwakamata wanaosingizia dini kutekeleza
mashambulizi.
No comments:
Post a Comment