Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena
kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia Mashabini wenzao wa
Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa
kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.lakini kwa hali ilivyo hivi sasa
Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza
kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani
hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa
chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa
Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani
kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na
Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshabiki wa Simba katika picha hii anaonekana aking'oa kiti na kukirusha upande mwingine. Huu sio utaarabu hata kidogo.
Mashabiki
wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga
kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
Viongozi
wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na
kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.
Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
Askari
Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda
kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa
Mashabiki wa Simba.
Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.
No comments:
Post a Comment