Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu masuala ya Muungano
katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini
Dodoma ljana.Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya Muungano katika
ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini
Dodomajana
Picha na Magreth Kinabo – MAELEZO
Na Magreth Kinabo- MAELEZO,DODOMA
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kwamba
Muungano wa Tanzania utakuwepo na utaendelea kudumu, hivyo hakuna mtu
atakayeweza kuuhujumu au kuuvunja kwa maslahi yake binafsi.
Aidha
Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema kauli iliyotolewa na Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar , Maalim Seif Sharrif Hamad hivi karibuni
kuwa Wanzanzibari wote wanataka Muungano wa Mkataba si kauli ya kweli
kwa kuwa hakuwahi kuzungumza na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
wala wananchi, hivyo wananchi wasitishike.
Kauli
hiyo imetolewa na Balozi Seif wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu masuala ya Muungano na mchakato wa Katiba Mpya katika
ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodoma
jana.
“Wanzanzibari wengi wanauthamini Muungano tungependa kuuendeleza na kuihimarisha kwa maslahi ya pande zote za Muungano.
“
Katika mchakato huu,tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa kuonesha dhahiri
ni zao za kutaka kuvuja Muungano kutokana na kauli zao . Kauli nyingi
zinatolewa zenye kuchonganisha wananchi wa pande mbili za Mujungano,
alisema Balozi Seif.
Alisema
kwa mfano ,kauli za kusema Wazanzibari wote hawataki Muungano wanataka
Mkataba “ Naomba kuuliza ni Wazanzibari gani hao wanaosemea mbona sisi
hapa pia ni Wazanzibari na hatuna msimamo huo wa mkataba? alihoji Balozi
Seif.
Akifafanua
swali lililoulizwa na mwandishi wa habari kuwa kauli aliyoitoa Maalim
Sief kuwa ni ya Serikali, Balozi Iddi alisema si kweli kuwa kauli hiyo
ni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“
Maalim Seif kasema kama Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) wala si
kwa niaba ya Serikali. Hakusema kama Makamu wa Pili wa Rais,”
alisisitiza Balozi Seif . Hivyo wananchi watambue kauli hiyo ni ya
uongo na hana uwezo wa kusema lolote.
Aliwataka
wananchi wa Zanzibar watambue kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
iko macho na yeyote atakayefanya fujo atashughulikiwa kikamilifu.
Alisema
Muungano una faida kwa Wazanzibari kuliko Watanzania Bara katika umoja
na kupanua wigo mpana wa matumizi ya ardhi,biashara na ajira.
Akizungumzia
kuhusu mchakato wa Katiba Mpya alisema unakabiliwa na changamoto za
kukosekana kwa uvumilivu miongoni wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Bunge hilo kutawaliwa na hisia za kisiasa badala ya maslahi ya Taifa na
kuna vikundi vya wachache wasiotaka mchakato huu uendelee kutokana na
utashi wa kisiasa.
“
Vitendo vya uvunjifu wa amani kila siku ili Bunge liahirishwe kwa
sababu tu za kibinafsi za baadhi ya wanasiasa si jambo jema hasa kwa
kuwa kodi ya Watanzania inapotea bila ya kufanya kazi iliyokusudiwa
kuifanya na sisi waheshimiwa wajumbe, “ alisema huku akisisitiza kuwa
hali hiyo haitaweza kustahimiliwa.
Balozi Sief alisema wako katika Bunge hilo kwa kutetea maslahi ya Watanzania na sio mtu binafsi.
Aliwataka
viongozi hao kuwa mfano mwema wa matendo mazuri mbel e ya jamii ya
Watanzania na kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kustahimiliana na
kuheshimiana ili lengo la Katiba Mpya liweze kutimia kwa maslahi ya
taifa na Watanzania .
Akifafanua
kuhusu makundi yaliyoundwa katika mchakato huo ambayo baadhi yao kuwa
ni Tanzania Kwanza na Ukawa kuwa si rasmi bali yameundwa kwa utashi
No comments:
Post a Comment