Mchungaji Kiongozi SILVANUS D. KOMBA (Punda wa yesu) akihubiri katika kanisa hilo.
SSP - PITER SIMA akitoa hotuba yake katika misa hiyo kwenye kanisa la mlima wa moto.
Mchungaji SILVANUS D. KOMBA akiwa katika maombi pamoja na Mkuu wa kikosi
cha usalama barabarani PITER SIMA - SSP mwenye tai ya mistari katika
kanisa hilo
Baadhi ya wanakwaya katika kanisa hilo wakiiombea nchi kwenye misa hiyo
Baadhi ya wanakwaya katika kanisa hilo wakiiombea nchi kwenye misa hiyo
Makanisa yamekumbushwa kuwaombea wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba Mpya ili waweze kudumisha amani, utulivu, mshikamano na
utengamano uliopo hapa nchini ili bunge hilo
lisiwe sababu ya kuwagawa watanzania kwa matabaka ya kidini, kisiasa na kichama.
Ushauri huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi
wa kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God SILVANUS KOMBA,kwenye ibada ya
kuliombea Bunge Maalum la Katiba na Taifa kwa ujumla iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo eneo la Sabasaba mjini Dodoma.
Alisema ili Wajumbe wa Bunge hilo wasiweze
kuigawa Taifa kwa itikadi za kichama, kidini na kisiasa ni muhimu Makanisa yakatumia
fursa zake kwa kueelekeza maombi kutoka ya Mungu ili kudumisha amani na utulifu
ndani la Bunge hilo.
Mchungaji huyo katika mahubiri yake
alisema kuwa kanisa hilo litaendelea kukemea kwa
nguvu zote wale wote wanaochochea kwa maneno machafu yanayolichafua Bunge hilo pamoja na wajumbe na
Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoa wa Dodoma Mrakibu mwandamizi wa Polisi PETER SIMA alisema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na serikali
ina imani kubwa na Makanisa katika kuombea Taifa na Bunge la Katiba ambalo hivi
sasa linaendelea kujadili Katiba Mpya.
SIMA akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP alisema kuwa makanisa yamekuwa yakifanya kazi
yake kwa malengo ya kuwabadilisha watu wenye tabia mbaya kuwaweka kwenye usalama.
Alisema kwa upande wa Jeshi la Polisi hao
kazi yao kuhakikisha inalinda usalama wa mali na watu wake, hivyo mambo yote hao
yakifanyika kwa pamoja Taifa linakuwa katika hali ya usalama na hatimaye hata kwa
Wajumbe wa Bunge wanakuwa salama.
“Ni imani yake kubwa katika maombi
yaliyofanyika na kanisa hili, Katiba inayojadiliwa itapatikana na itawagusa Watanzania
wote kutokana na juhudi za makusudi zinazofanyika ambazo waumini wamekuwa
wakijitoa kwa ajili ya maombi” alisema Sima.
No comments:
Post a Comment