Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 18, 2014

Mawaziri Wasitokane na wabunge


NA Zamaradi Kawawa, Maelezo Dodoma.

Mwenyekiti aw Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ameliambia bunge Maalum la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma kuwa Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge.

Amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.

Amesema Mawaziri watateuliwa na Rais NA kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo NA ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa NA vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri NA wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.


 

No comments:

Post a Comment