Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 20, 2014

Mgogoro Ziwa Nyasa sasa kuamuliwa Leo Maputo

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe.
Maamuzi ya mwisho ya usuluhishi wa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi yanatarajiwa kutolewa kesho na kutwa.
Mchakato wa kesi yake hadi sasa umedumu kwa takribani miaka miwili sasa.
Maamuzi ya mwisho ya usuluhishi huo yanatarajiwa kufanywa na jopo linaloundwa na Marais wastaafu watatu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini na Mashariki mwa Afrika ambao ni Mwenyekiti waka ni Joachim Chissano (Msumbiji), Thabo Mbeki (Afrika Kusini) na Festus Mogae (Botswana), huku wakishirikiana na wanasheria na wataalam wa masuala ya migogoro ndani ya jumuiya hiyo.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga, alisema jopo hilo la usuluhishi wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, katika Ziwa Nyasa, linatarajia kutoa taarifa rasmi ya usuluhishi kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho hadi kesho kutwa katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.
Mbali na jopo hilo, pia mawaziri wa Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kutoka nchi za Tanzania na Malawi, wanatarajia kuhudhuria kikao hicho nyeti cha siku mbili kwa ajili ya kupokea taarifa hiyo ya maamuzi ya mwisho ya usuluhishi.
Jopo la wataalam na wanasheria wa masuala ya mipaka toka ndani ya jumuiya hiyo ambao watashirikiana na Marais hao wastaafu katika kutoa hatima ya usuluhisho huo linaundwa na Jaji Raymond Ranjeva, Jaji mstaafu wa ICJ; Profesa George Kanyeihamba, Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Uganda na Jaji Baney Afako, Mshauri wa Masuala ya Sheria kwenye Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa mpaka wa Sudan. 
Wengine ni Profesa Martin Pratt, Mkurugenzi wa Utafiti wa Jiografia na Mipaka; Dk. Dire David Tladi, Mjumbe wa Kamisheni ya Sheria ya Umoja wa Mataifa; Miguel Chissano, Kiongozi wa Chuo kinachoshughulikia mipaka ya Baharini na Nchi Kavu pamoja na Dk. Gbanga Oduntun, Profesa wa Sheria na Mjumbe wa Kamisheni ya mgogoro wa mpaka kati ya Nigeria na Cameroon.
Kabla ya kufanyika kwa matukio hayo mawili mjini humo mwezi uliopita, Tanzania na Malawi kwa nyakati tofauti, ziliitwa na jopo hilo kuhojiwa juu ya taarifa zao za ushahidi wa umiliki halali wa ziwa hilo zilizowasilisha kwao na mawaziri wa mambo ya nje na wa pande hizo mbili Novemba, mwaka jana.
Julai, mwaa juzi, Rais wa Malawi, Joyce Banda, mara baada ya kuapishwa kushika kiti hicho kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliibua mgogoro huo kwa kutoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la Ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania, kwa madai ya kwamba ziwa hilo lote lipo upande wake.
Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi, unaotambuliwa na sheria za kimataifa ni ule unaopita kati ya ziwa hilo, ambao ulianza kutumiwa na raia wa nchi hizo mbili miaka mingi iliyopita kwa kila upande kumiliki asilimia 50 ya Ziwa.

No comments:

Post a Comment