Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, March 2, 2014

MWENYEKITI UVCCM ASHAMBULIWA KWA RISASI TAZAMA PICHA

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM, kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”


Click image for larger version. 

Name: IMG-20140301-WA0071.jpg 
Views: 0 
Size: 71.7 KB 
ID: 142391 

Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.
Matukio ya vurugu na vitisho vimeanza kutawala kwa kasi kubwa katika ulingo wa Siasa za ndani hapa nchini kwetu, ni vyema sasa Serikali ikawa macho katika kuangazia upande wa Siasa kama eneo hatari (Danger Zone) ili kulinda Uhai wa Vijana na wananchi kwa Ujumla.

Click image for larger version. 

Name: IMG-20140301-WA0073.jpg 
Views: 0 
Size: 84.1 KB 
ID: 142389 

Click image for larger version. 

Name: IMG-20140301-WA0072.jpg 
Views: 0 
Size: 44.6 KB 
ID: 142390 
Click image for larger version. 

Name: IMG-20140301-WA0091.jpg 
Views: 0 
Size: 46.4 KB 
ID: 142395 
Click image for larger version. 

Name: IMG-20140301-WA0068.jpg 
Views: 0 
Size: 122.2 KB 
ID: 142388

No comments:

Post a Comment