Katika hali isiyo ya kawaida jioni hii
kumetokea vurugu katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wakati
wa mchezo kati ya Timu ya Stand United ya Shinyanga na Polisi ya mkoani
Mara ambapo wenyeji wa mchezo huo Stand United waliibuka washindi kwa
bao moja dhidi ya Polisi.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema
vurugu hizo zimetokea mara baada ya mchezo kuisha,ambapo wachezaji wa
timu ya Polisi Mara walipotoka uwanjani walimfuata refa wa mchezo huo
pamoja na wasaidizi wake kutaka kumpa kichapo,na kufuatia hali hiyo
baadhi ya watu waliokuwa katika eneo hilo wakiwemo wachezaji wa timu ya
Stand united waliingia uwanjani kutaka kumsaidia refa ili asipigwe.
Kati ya watu walioingia uwanjani hapo,aliyekuwa mbele alikamatwa na askari polisi waliokuwa eneo hilo na ndipo vurugu zikaanza na askari hao wanaosemekana kuwasaidia POLISI WENZAO wakaanza kurusha mabomu ya machozi katika eneo la jukwaa kuu ambako alikuwepo pia mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini hapa nchini.
Kufuatia vurugu hizo baadhi ya watu
waliokuwa eneo la jukwaa kuu akiwemo mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini
Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini wamejeruhiwa katika
sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na purukushani za hapa na pale
mabomu hayo ya machozi kwani wengine walikuwa wanaanguka hovyo.
Akizungumza mara baada ya vurugu hizo
naibu waziri wa madini Stephen Masele amesema vurugu hizo zimetokana na
askari polisi waliokuwa wanawasaidia polisi wenzao yaani timu ya
Polisi,walioshindwa kumdhibiti kijana aliyekuwa anakwenda kumsaidia
refa.
Masele amesema ni vyema TFF ikaaangalia
namna ya kupunguza timu za polisi kwani ziko nyingi sana na wanalindana
matokeo yake kusababisha vurugu leo mjini Shinyanga
No comments:
Post a Comment