Na. Abdulaziz Video, Lindi
Mafuriko yaua na kusitisha usafiri Lindi Masasi,Ruangwa na Nachingwea ikiwemo Newala na Tandahimba Mkoani Mtwara
Watu Wanne wamefariki dunia katika wilaya ya Lindi kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa Tarehe 26 na 27 /3/2014 na kusababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Lindi, Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi
Sambamba na mvua hizo licha ya kupoteza maisha ya watu hao na wengine kujeruhiwa pia Imesitisha huduma za usafiri kati ya Lindi, Masasi, Nachingwea, Ruangwa na Newala kufuatia kukatika kwa madaraja ya Mtama na Nyangao pamoja na makazi ya wananchi wanaoishi pembezoni kulikosababishwa na kufurika kwa mto Lukuledi.
Akiongea na globu hii mara baada ya kukagua athari hizo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila alieleza kuwa Tayari Wakala wa barabara Mkoa wa Lindi inafanya jitihada za haraka kuweka njia ya Muda ili kuokoa wananchi wengi waliokwama katika maeneo hayo ili kupunguza msongamano uliopo Sambamba hilo Mwananzila alitoa wito kwa baadhi ya wananchi waliopo maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo kutoruhusu watoto wao kucheza katika mto huo kutokana na ongezeko kubwa la maji.
Aidha Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi aliwahakikishia usalama abiria wote waliokutwa na maafa hayo kuwa Jeshi la polisi limejipanga kutoa ulinzi wakati wote katika maeneo hayo huku akitoa agizo kwa wenye mabasi ya Abiria kutofanya safari hadi kutakapokamilika kwa maeneo hayo ili kupunguza idadi kubwa ya wasafiri.
Kukatika kwa madaraja hayo tayari kumesitisha Usafiri kwa wanaotoka Mkoa wa Lindi kwenda wilaya za Masasi, Nachingwea, Tunduru, Ruangwa, Liwale, Nanyumbu, Newala
No comments:
Post a Comment