Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 20, 2014

RATIBA YA CAF CHAMPIONS LEAGUE RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 KUANZA KUANZA IJUMAA

MASHINDANO MAKUBWA YA KLABU BARANI AFRIKA, CAF CHAMPIONZ LIGI, IJUMAA YANAINGIA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16 ILI KUPATA TIMU 8 AMBAZO ZITAINGIA KWENYE DROO KUPANGA MAKUNDI MAWILI YA TIMU 4 KILA MOJA.


Mabingwa Watetezi, Al Ahly ya Misri, ambao Raundi iliyopita waliwatoa Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, kwa Mikwaju ya Penati baada kwenda Sare ya Jumla ya Bao 1-1 katika Mechi mbili, wataanza kucheza Ugenini huko Libya na Klabu ya Al Ahli – Benghazi.
Nao TP Mazembe ya Congo DR, Klabu yenye Mastraika wawili Mashujaa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, itakuwa Ugenini huko Ivory Coast kucheza na Sewe Sport.
Mechi nyingine zenye mvuto ni ile kati ya Nkana FC ya Zambia na Magwiji wa Egypt, Al Zamalek itakayochezwa huko Zambia..
Klabu nyingine ya Congo DR ni AS Vita ambayo itakuwa Nyumbani kucheza na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Marudiano ya Mechi ya Raundi hii ni Wikiendi ya Machi 28.


CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Ijumaa Machi 21

16:00 Al Ahli - Benghazi – Libya v Al Ahly - Egypt     

16:00 Nkana FC – Zambia v Al Zamalek - Egypt

19:30 AS Bamako РMali v Esp̩rance Sportive de Tunis РTunisia

Jumapili Machi 23

16:30 AS Vita Club - Congo, DR v Kaizer Chiefs - South Africa

16:50 AC Leopards de Dolisie – Congo v Al-Hilal - Sudan

19:00 Sewe Sport - Ivory Coast v TP Mazembe - Congo, DR

19:30 Horoya Athl̩tique Club РGuinea v Club Sportif Sfaxien - Tunisia

21:15 Entente Sportive de Sétif - Algeria v Coton Sport FC - Cameroon

No comments:

Post a Comment