Mamlaka ya usalama wa safari za
baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya
shirika la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya
hewa na mawimbi makali baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua
kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza
kupaa kwa usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la
wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa
kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.Dr Erik van Sebille, ambaye ni mtaalam wa maswala ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini Sydney, amefanya utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua ni wapi na vipi vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa vigumu sana kupata mabaki ya ndege hiyo.
Kadhalika amesema kuwa vifusi vilivyoenekana hapo jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi makali.
"Haitakuwa rahisi kabisa kupata kijisanduku cha kunasa habari. Mawimbi ya eneo hili ni makali na kwa hiyo vifusi ambavyo wametambua kwa sasa huenda vimehamishwa katika kipindi cha majuma mawili au matatu tangu ndege hiyo ianguka-na huenda vimesafiri kilomita alfu moja tayari. Na hii inaifanya vigumu kurejelea utafutaji kwa sababu bahari inabadilika sana hapa-ina vurugu ukipenda."
Hapo awali naibu waziri wa mashauri ya nchi za Kigeni wa China Xie Hangsheng, aliitaka serikali ya Malaysia kutoka ushahidi unaoelezea kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo la Kusini mwa bahari Hindi. Ndege hiyo ilitoweka kwenye mtambo wa Radar zaidi ya majuma mawili yaliyopita
No comments:
Post a Comment