
CHADEMA JIMBO LA CHALINZE
TAARIFA KWA UMMA
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza
mchakato wa ndani wa kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo
unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za
uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi Jimbo, kuanzia tarehe 4 Machi na
mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa tarehe 7 Machi 2014,
saa 10.00, jioni.
Kura
za maoni ndani ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa
Chalinze na kufuatiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo ili
kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya chama na hatimaye kikao
cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili kupata mgombea
atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.
Mpaka
sasa wagombea waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na
wagombea wengine watatu (3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya
Chama, Dar es Salaam, hivyo hadi sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa
rasmi ni sita.
Tunatumia
nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA,
kuwa fomu za kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu
tatu, Makao Makuu ya Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti
ya chamawww.chadema.or.tz
Imetolewa Machi 5, 2014
Iddi Omary Ucheche
Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Chalinze

No comments:
Post a Comment