Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
|
Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma
Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na mpango wa kuanzisha ubalozi Tanzania Nchini Korea.
Hayo yamesemwa leo na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelewa na Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Mjini Dodoma leo.
Spika Makinda alisema kuwa serikali itaendelea kulisimamia suala hili ikiwa ni njia moja wapo ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
“Tuna kila nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania nchini Korea na hii tunafanya tukiwa na nia ya kuendelea kuujenga uhusiano kati yetu” Alisema Spika Makinda.
Aidha Spika Makinda alisema kuwa bunge la Tanzania limeweka mikakati mbalimbali ili kuliimarisha na kulifanya kuwa la kimataifa ikiwamo kuridhia uanzaji wa bunge la kimtandano (E-parliament).
Akizungumzia kuhusu uanzishaji wa Radio ya Bunge Spika Makinda spika alisema kuwa bunge linampango wa kuwa na Radio ya bunge ili kupunguza gharama za kutumia radio za taifa kama wanavyofanya sasa.
Pia Spika Makinda alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon kushirikiana katika kuanzisha chama cha ushirikiano cha wabunge wa Korea na Tanzania.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano ambaye ni mbunge wa bunge la Korea Bw. Ahn Hong Joon, alimuahidi Spika Makinda kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwamo mpango wa Tanzania kuwa na Bunge la kimtandao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa alishukuru Serikali ya Korea hasa kutokana na Misaada mbalimbali wanayopata kutoka Serikali ya Korea ikiwamo ujenzi wa chuo cha Afya na Ujenzi wa Daraja la Malagarasi |
|
No comments:
Post a Comment