Mazungumzo
ya Tanzania na Malawi yaliyokuwa yakifanyika katika mji mkuu wa
Msumbiji Maputo, yamemalizika na pande mbili kufikia makubaliano
kuhusiana na mzozo wao wa mpaka katika Ziwa Nyasa.
Joaquim
Chissano Rais wa zamani wa Msumbiji ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa
mazungumzo hayo amesema kuwa, Tanzania na Malawi zimetofautiana namna ya
kuupatia ufumbuzi mzozo huo. Amesema kuwa, katika hali ambayo Tanzania
inasisitiza juu ya kuainishwa mpaka, Malawi inatilia mkazo zaidi suala
la vyanzo vya utajiri.
Timu za
mazungumzo za Tanzania na Malawi zilikutana tena mjini Maputo Msumbiji
baada ya mazungumzo ya awali yaliyofanyika mwaka jana huko Lilongwe
Malawi kutokuwa na natija. Kwa muda sasa Tanzania na Malawi zimekuwa
zikisuguana kuhusiana na mpaka katika Ziwa Nyasa. Nchi hizo, kila moja
inadai kwamba, Ziwa Nyasa ni miliki yake. Hadi sasa juhudi za upatanishi
zenye lengo la kuhitimisha mzozo huo wa mpaka ambao unatishia
mustakbali wa kidiplomasia kati ya nchi mbili hizo bado hazijazaa
matunda.
No comments:
Post a Comment