Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 31, 2014

TAZAMA PICHA ZA SHEREHE YA MIAKA 30 YA NDOA YA MWALIMU CHRISTOPHER NA DIANA MWAKASEGE ILIVYOKUWA

Shangwe za GK leo zipo kwa mwalimu Christopher na Diana Mwakasege ambao mwezi huu basi wamefikisha miaka 30 ya ndoa yao. Ambapo kulikuwa na tafrija fupi ya kusherehekea tendo hilo iliyofanyika jijini Arusha wiki iliyopita ambayo ilihudhuriwa na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Askofu dkt Alex Gehaz Malasusa, familia ya mwalimu Mwakasege, ndugu, jamaa pamoja na marafiki. Mungu aendelee kuwainua watumishi hawa ambao wamekuwa baraka kwa taifa letu la Tanzania. GK inawapongeza sana na kuwatakia maisha marefu zaidi ya ndoa pamoja na baraka zitokazo kwa Mungu ziambatane pamoja nanyi siku zote mkazidi kupata maarifa zaidi katika kuwahudumia watu wake
Meza kuu.
Wageni waalikwa mabibi na mabwana.
Ndafu walikuwepo bagwetu.
The Voice wakiimba katika sherehe hiyo.

Keki, huku wengine wakishuhudia.
Picha za tukio ambazo GK imefanikiwa kuzipata.


Mwalimu Mwakasege, mkewe pamoja na mtoto wao wa kiume.
Waalikwa wakiwapokea kwa shangwe maharusi.
Mwalimu Christopher na Diana Mwakasege.PICHA NA GK



No comments:

Post a Comment