Ikiwa ni muda mfupi tangu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuthibitisha kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Jack Wilshere kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 8 baada ya kuvunjika mguu, mashabiki wa timu ya Tottenham wamemtengenezea kitu walichoita ‘zawadi’ Wilshare.
Wilshare ambaye amekuwa akiandamwa sana na majeraha tangu alipoanza kukichezea kikosi cha wakubwa cha Arsenal, amevunja mfupa mdogo wa mguu wake wa kulia.
Katika kuendeleza utani wa jadi mashabiki wa Tottenham wamemtengenezea Jack Wilshare kiti cha kukalia watu wasioweza kutembea kwa miguu (wheelchair).
Arsenal inacheza na Everton katika FA Cup kesho, kisha wataenda kucheza na Bayern Munich katika champions league, na baada ya hapo watakutana na Tottenham katika EPL
No comments:
Post a Comment