Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 31, 2014

WAFANYAKAZI SHOPRITE KULIPWA MADAI YAO



image

CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kimesema wafanyakazi wa Shoprite watalipwa stahili zao zote Machi 31, mwaka huu.
Akizungumza na wafanyakazi wa Shoprite jijini Dar es Salaam jana, Katibu Msaidizi Sekta ya Biashara TUICO, Pales Jonathan alisema kuwa, wamezungumza na mwajiri wa Shoprite, akaahidi atalipa stahili zao zote akishalipa ndiyo ataondoka.
Alisema kuwa, wamekaa kwenye meza ya mazungumzo na mwajiri wa Shoprite, hivyo hawezi kuuza maduka yake kwa mtu mwingine mpaka atakapomaliza kulipa madeni ya wafanyakazi.
Jonathan aliwataka wafanyakazi wa Shoprite kuendelea na kazi bila wasiwasi kwani mwajiri mpya ambaye ananunua maduka hayo NAKUMATT ataajiri wafanyakazi wote wa Shoprite na atakapoanza wataingia mkataba mpya na ameshakubali.
Alisema kuwa kama bado hawajafikia mwafaka wa kuyakabidhi maduka hayo wataendelea kufanya kazi kama kawaida na watalipwa mishahara yao na muda wa ziada baada ya kazi.
Hata hivyo alisema, kama kibali cha kukabidhi maduka hayo hakijatoka kutoka Tume ya Ushindani (FCC) wataendelea kufanya kazi na watalipwa kwa siku hadi hapo kibali kitatoka.chanzo Majira


 

No comments:

Post a Comment