Msafara
wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans leo asubuhi umeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mjini
Morogoro tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumamosi, mechi
itakayopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Young
Africans inayonolewa na makocha Hans Van der Pluijm kutoka Uholanzi,
Charles Mkwasa na Juma Pondamali wazawa jana jioni ilifanya mazoezi
katika Uwanja wa Kaunda ikiwa ni masaa 10 baada ya kuwasili kutokea
jijini Cairo ilipocheza dhidi ya Al Ahly katika mashindano ya Klabu
Bingwa barani Afrika.
Kuhusu
mchezo wenyewe Kocha Hans amesema haifahamu vizuri timu ya Mtibwa Sugar
lakini kwa kushirikiana na wenzake wamejiandaa kuhakikisha timu
inafanya vizuri na kupata pointi 3 katika mchezo huo, yaliyotokea Misri
yameshapita sasa kilichobakia ni kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu.
Kwa
mujibu wa daktari wa timu ya Young Africans Dr Suphian Juma amesema
wachezaji wote wapo fit kuelekea kwenye mchezo huo na mchezaji pekee
atakayekosena ni Mrisho Ngasa ambaye alipata maumivu ya nyama za paja
hivyo kwa sasa bado anaendelea na matibabu huenda akaanza mazoezi na
wenzake mwishoni mwa wiki hii.
Mechi
dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumamosi itafungua ukurasa mzuri kwa
Young Africans kwani endapo itashinda mchezo huo itarejea kwenye kiti
cha uongozi wa Ligi Kuu na kujitengenezea mazingira mazuri ya kutetea
Ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Msafara
umeondoka ukiwa na idadi ya watu 31 wakiwemo wachezaji 22 pamoja na
benchi la Ufundi ambapo leo jioni timu inatarajiwa kufanya mazoezi mjini
Morogoro kabla ya kesho kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kuelekea siku
ya mechi.
Wachezajii waliondoka ni:
Walinda Mlango: Deo Munish "Dida", Juma Kaseja na All Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani na Ibrahim Job
Viungo: Frank Domayo, Athumani Idd "Chuji", Nizar Khalfani, Hassan Dilunga na Haruna Niyonzima
Washambuliaji: Saimon Msuva, Said Bahanuzi, Hamis Kizza, Emmanuel Okwi, Didier Kavumbagu, Hussein Javu na Jerson Tegete
No comments:
Post a Comment