skip to main |
skip to sidebar
YANGA YAWASILI ALEXANDRIA, KUFANYA MAZOEI USIKU
Wachezaji wa Young Africans wakiwasili katika Hoteli ya Sheraton
Msafara
wa kikosi cha Young Africans umewasili salama jijini Alexandria leo
majira ya saa 7 na kufikia katika hoteli ya Shaeraton ukitokea katika
jiji la Cairo ambako awali mchezo wa marudiano ulipangwa kufanyikwa
kabla ya jana kutolewa mabadiliko ya uwanja na mchezo huo utachezwa
kesho katika dimba la Uwanja wa El Max Stadium jijini Alexandria.
Young Africans ambayo iliwasili juzi jijini Cairo na kuweka kambi
katika hoteli ya Nile Paradise Inn na kufanya mazoezi kwa siku mbili
mfululizo katika uwanja uliopo ndani ya hoteli hiyo ambayo uongozi wa
Young Africans kwa kushirikiana na Ubalozi uliweza kufanikisha kambi
hiyo.
Awali makamu mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga
alitangulia jijini Alexandria jana asubuhi pamoja na maofisa wa ubalozi
kwa ajili ya kufanya maaandalizi ya sehemu ambapo timu itafikia na leo
timu ilipofika ilikuta kila kitu kmeshakaa kwenye mpangilio wake.
Mara
baada ya kuwasili jijini Alexandria wachezaji na viongozi wa Young
Africans wamepata chakula cha mchana kisha wamepata mapumziko mpaka
majira ya saa 12 jioni ambapo timu itakwenda uwanja wa El Max kwa ajili
ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo.
Morali
ya wachezaji bado ni ya hali ya juu kuelekea mchezo huo wa kesho, haki
ya kambi ni nzuri hakuna majeruhi hata mmoja hivyo vijana wote wapo tayari kwa kesho kuipeperusha bendera ya nchi.
Jioni timu itafanyya mazoezi katika Uwanja wa El Max ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho.
No comments:
Post a Comment