Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 3, 2014

KESI YA ZITTO KABWE DHIDI YA CHADEMA YASOGEZWA HADI MEI 29 MWAKA HUU.



KESI ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto dhidi ya chama hicho, imeahirishwa hadi Mei 29 mwaka huu, itakapotajwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
 
Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi aliahirisha kesi hiyo jana kwa kuwa Jaji John Utamwa anayeisikiliza, anaumwa.
 
Katika kesi hiyo, Zitto anaomba Mahakama itoe zuio kwa Kamati Kuu au chombo chochote cha chama, kujadili uanachama wake hadi atakapokata rufaa ya kupinga uamuzi uliomvua uongozi wa chama. Anaomba Mahakama imwamuru Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa.
 
Ampe nakala zinazotoa sababu za uamuzi wa kumvua uongozi katika kikao kilichofanyika Novemba 22 mwaka jana, ili akate rufaa katika Baraza Kuu la Chama.
 
Aidha, anaomba mahakama iamuru Chadema isiingilie kazi zake za ubunge wala uanachama wake.
 
Zitto amefungua kesi hiyo dhidi ya Baraza la Wadhamini la chama hicho na Dk Slaa. Kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa, Mahakama ilitoa amri kwa Kamati Kuu au chombo chochote cha Chadema, kutojadili uanachama wa Zitto hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIII

No comments:

Post a Comment