Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 16, 2014

MELI YAZAMA IKIWA NA ABIRIA 460

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.
Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja ilioyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji , zimepelekwa katika ferry moja inayozama kusini mwa pwani hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea.
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kusakama maji zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea huku duru zikidhibitisha kuwa mtu mmoja amepatikana ameaga dunia

No comments:

Post a Comment