Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 4, 2014

MKUU WA MKOA WA DAR AMPASHA JOHN MNYIKA....ADAI HAWEZI KUSITISHA AGIZO LAKE LA PIKIPIKI NA BAJAJ KUINGIA KATIKATI YA JIJI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amesema hawezi kusitisha agizo lake la pikipiki na bajaj kuingia katikati ya jiji, kwani hana mamlaka hayo, kwani anasimamia sheria. 
Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na Habari leo  kuhusu ombi la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kutaka asitishe agizo hilo kupisha mazungumzo baina ya Serikali, wahusika wa bodaboda na bajaj na wadau wengine muhimu kupata ufumbuzi.
Sadiki alisema hana habari na suala hilo la Mnyika na kuwa agizo hilo si yeye, bali ni sheria na anaisimamia kama inavyotakiwa.
“Kwanza sijapata barua hiyo ya Mnyika…sijui maudhui yake ni yapi… mimi ni msimamizi tu wa sheria,” alisema Sadiki na kuongeza kuwa hata Mnyika kama Mbunge, analifahamu hilo.
Aidha, kuhusu mipaka ya eneo la katikati ya jiji (CBD), Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu ( Sumatra), David Mziray aliitaja mipaka hiyo hiyo.
Mziray alifafanua kuwa mipaka ya CBD kwa barabara ya Morogoro mwisho ni Ubungo, barabara ya Uhuru mwisho ni Buguruni, Barabara ya Nyerere ni Tazara na barabara ya Kilwa ni eneo la Chuo cha Uhasibu, ambapo zaidi ya hapo vyombo hivyo havitakiwi kuingia mijini.
Kuhusu madai ya Mnyika, Mziray alisema agizo la kupiga marufuku pikipiki na babaj kuingia maeneo ya mijini limekuwa na mgogoro, baina ya wanaofanya kazi hiyo na vyombo vya ulinzi na usalama.
Alisema kutokana na agizo hilo, watumiaji wa kawaida wa vyombo hivyo wamekuwa wakipata usumbufu wa kukamatwa na kusumbuliwa, wakidhaniwa kwamba ni sehemu ya biashara ya usafiri kwa kutumia bodaboda na bajaji.
Aidha, alisema amri hiyo imezusha usumbufu kwa abiria, ambao wanaotumia vyombo hivyo vya usafiri, kama mbadala wakati wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo kwa Haraka (BRT).
Mnyika alisema katika kufuatilia suala hilo, ofisi yake kupitia kwa Katibu Msaidizi, Aziz Himbuka tayari imeshafanya mawasiliano na viongozi wa waendesha bodaboda katika Manispaa ya Kinondoni kupata maelezo na vielelezo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Alisema vilevile amemwandikia ujumbe Mkuu wa Mkuu wa Mkoa, kusitisha kwa muda utekelezaji wa agizo hilo, kupisha mazungumzo baina ya Serikali, wahusika wa bodaboda na bajaj na wadau wengine muhimu ili kupata ufumbuzi.


Alitaka Halmashauri ya Jiji na Manispaa za Ilala na Kinondoni, kuweka wazi mipaka ya eneo la katikati ya Jiji na pia kuweka utaratibu bora zaidi wa usafiri wa kuingia katikati ya mji, wenye kuzingatia maslahi ya wasafiri na fursa ya vijana kuweza kujiajiri.CHANZO HABARI LEO

No comments:

Post a Comment