Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 2, 2014

Mugabe asusia mkutano kuhusu CAR

Maelfu ya waisilamu wametoroka vita CAR na kukimbilia nchi jirani ya CAR
Viongozi wa Ulaya na Afrika wanatarajiwa kuanza kujadili mgogoro unaotokota katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, katika mkutano maalum unaofanyika kando na kongamano la viongozi wa Ulaya mjini Brussels.
Rais Robert Mugabe amesusia kongamano hilo baada ya Muungano wa Ulaya kukataa kumwondolea marufuku ya muda ya Visa mkewe Grace.
Bwana Mugabe aliungwa mkono na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye pia ameamua kuususia mkutano huo kama ishara ya kumuunga mkono Mugabe.
Zuma alisema kuwa muda umewadia wa Ulaya kukoma kuwaangalia waafrika kama sio watu.
Muungano wa Ulaya tayari umezindua kikosi cha jeshi lake nchini CAR, na kuelezea mipango yake kutuma wanajeshi 1,000 kuwasaidia wanajeshi wa Afrika na wale wa Ufaransa wanaoshika doria nchini humo.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa waisilamu 19,000 wanakabiliwa na tisho la kuuawa nchini humo.
Maswala ya Uchumi na Uhamiaji pia yatapewa kipaombele kwenye mkutano huo.
Viongozi 30 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano lenyewe wakiwemo marais wa Afrika.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon atahudhuria mkutano kuhusu CAR pamoja na viongozi wa Afrika na wale wa Muungano wa Ulaya.
Ameahidi kufAnya kila awezalo kuhakikisha anaimarisha juhudi za kukabiliana na migogoro ya kimataifa.CHANZO BBC
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII

No comments:

Post a Comment