Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 3, 2014

PICHA ZA MATUKIO KUTOKA DODOMA LEO KAMATI ZA BUNGE LA KATIBA WAKIENDELEA NA KAZI

 Mwenyekiti wa Kamati namba sita ya Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira(katikati) akisoma dua ya kuharisha kikao cha Kamati leo mjini Dodoma. Wengine ni Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari(kushoto).
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Jussa akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kwa Mwenyekiti wa wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(hayupo pichani)wakati alipotembelea Kamati namba Sita kujionea maendeleo yaliyokwishafikiwa katika kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya Katiba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kangi Lugola akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kwa Mwenyekiti wa wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(hayupo pichani)wakati alipotembelea Kamati namba Sita kujionea maendeleo yaliyokwishafikiwa katika kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Bunge hilo Godbless Lema(kushoto) leo mjini Dodoma wakati akitembelea Kamati mbalimbali kujionea maendeleo ya uchambuzi wa vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya kwa sura ya Kwanza na Sita.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Freeman Mbowe  akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kwa Mwenyekiti wa wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(hayupo pichani)wakati alipotembelea Kamati namba Saba kujionea maendeleo yaliyokwishafikiwa katika kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya Katiba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Benadetha Mshashu akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kwa Mwenyekiti wa wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(hayupo pichani)wakati alipotembelea Kamati namba saba kujionea maendeleo yaliyokwishafikiwa katika kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba Sita (6) ya Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati akitembelea Kamati mbalimbali kujionea maendeleo ya uchambuzi wa vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya kwa sura ya Kwanza na Sita. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stephen Massato Wassira(katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari(kushoto)
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma  kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba  baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) na Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia)

Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia).

No comments:

Post a Comment