Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 23, 2014

PICHA ZA MAZISHI YA DC MOSHI CHANG'A MKOANI IRINGA LEO

 Utaratibu  wa mazishi  ukiwekwa
 Waombolezaji wakiwa na majonzi
 Jeneza la mwili wa marehemu
 Spika Makinda akitoa  mkono wa pole kwa wafiwa
 pika Makinda  kulia akimpa pole waziri Hawa Ghasia
 Spika Makinda  akiwapa pole  wafiwa
 Spika  wa bunge Anne Makinda akiwa amepiga magoti  kuwapa  pole  wafiwa katika msiba wa aliyekuwa DC wa kalambo Moshi Chang'a leo mjini Iringa
 Spika wa bunge Anne makinda akisaini kitabu cha maombolezo ya DC Chang'a leo
 Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akitoa  salama zake na za Chadema pamoja na ubani wa TSh 100,000
 Wakuu wa  wilaya  mbali mbali nchini  wakiwa  wameubeba mwili wa DC mwenzao Moshi Chang'a leo
 Wakuu wa wilaya na wananchi  Iringa  wakiwa  wamebeba mwili wa Dc Chang'a mjini Iringa leo
 Wakuu wa wilaya na wananchi  Iringa  wakiwa  wamebeba mwili wa Dc Chang'a mjini Iringa leo
Mwili wa DC Chang'a ukipelekwa msikiti wa Mwanchang'a Kihesa 
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia leo  amemwakilisha  waziri  mkuu Mizengo Pinda katika mazishi  ya  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Marehemu Moshi Chang'a.

Katika mazishi  hayo yalihudhuriwa na mamia  ya  wakazi  wa Manispaa ya  Iringa na viongozi  wa serikali  kutoka mikoa mikoa  mbali mbali nchini pia  spika  wa  bunge Anne Makinda  alitumia nafasi hiyo  kuueleza  umma siri  nzito  iliyofichika  dhidi yake ya marehemu Chang'a mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza  ulioshirikisha vyama  vingi kuwa bila marehemu huyo asingeweza kuwa mbunge kutokana na kubanwa na chama cha upinzani cha NCCR Mageuzi kwa  kipindi  hicho


"Mimi  nimekuwa kwa niaba yangu mwenyewe na  jimbo la Njombe  kusini ambalo mimi ni mbunge  wake ....mwaka  1995 marehemu  alikuwa ni katibu  wa CCM Njombe na ndio mwaka  ambao  mfumo wa vyama  vingi  ulianza na yeye ndie  alikuwa katibu  na jimbo hilo  upinzani  ulilizingira kweli na hata kwa kukanyanga mguu kulikuwa hakuna  ila bila Chang'a kweli jimbo  hilo   niseme ukweli  lingekuwa limechukuliwa na Upinzani na kwa kipindi hicho chama chenye nguvu zaidi  kilikuwa ni NCCR Mageuzi "

Akizungumza   wakati wa kutoa  salama  mbali mbali kwa  viongozi  mjini  Iringa Spika Makinda  alisema  kuwa kwa mara ya kwanza  mwaka 1995  alibanwa kupita  kiasi na  NCCR Mageuzi  katika jimbo lake la uchaguzi la Njombe kusini na  kuwa  bila marehemu  huyo ambae kwa kipindi  hicho alikuwa ni katibu wa CCM wilaya ya Njombe kamwe asingeweza kuwa mbunge .

Mkuu wa  mkoa  wa Rukwa injinia Stella Manyanya  alisema kuwa  mkoa  wake amempoteza  kiongozi mzalendo na aliyependa kazi yake na kuwa hata  akiwa  safarini hakuwa na shaka na utendaji kazi wa mkuu  huyo wa  wilaya na kuwa  siku  zote mbali ya kuongoza kama kiongozi wa serikali ila wakati mwingi alitumia  kuwahubiria upendo  wananchi wa  wilaya  yake.

Kwani  alisema kuwa alikuwa hawezi kuanza mkutano  bila kumhubiri  mwenyezi Mungu mbali ya kuwa  yeye alikuwa muumini wa dini ya Kiislam ila alikuwa akihubiria dini ya kikristo  .

Hata  hivyo  alisema kuwa  hadi  kesho anaamini  alishinda  ubunge  jimbo hilo mwaka 1995 si kwa uwezo wake  bali  alishinda kwa uwezo wa marehemu Chang'a ambao  alionyesha  uwezo mkubwa  wa kumnadi na hata kufanikiwa  kuwa mbunge wa  jimbo hilo na leo  kuwa  spika wa bunge .

Alisema  iwapo  angekwama  kuwa  mbunge  mwaka 1995  basi yawezekana leo asingekuwa spika kwani angekuwa amekata tamaa ama angekuwa mbunge  mwingine katika jimbo hilo.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA FRANSIS GODWIN IRINGA

No comments:

Post a Comment