Baadhi
ya Watanzania waishio katika mji wa Shanghai nchini China
wamesherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania kwa
kukutana pamoja na kuzungumza mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Licha ya
sherehe hizo za Miaka 50 ya Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga baadhi
ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kumaliza mwaka huu.
Baadhi
ya Watanzania waishio Shanghai wakipiga picha ya pamoja katika shamra
shamra za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanzania,yaliyofanyika
jana.
Baadhi ya Watanzania wanaomaliza masomo yao mwaka huu wakipiga picha ya pamoja mbele ya keki ya Muungano.
Mmoja
wa wahitimu Bi. Hellen Shayo akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa
Watanazania waishio Shanghai cha kuwa mwanachama hai kwa kipindi chote
alichokuwa hapa.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria sherehe za Muungano.
Watanzania wakikata keki ya Muungano huku wakiwa wa nyuso za bashasha zinazodhihirisha umuhimu wa siku hiyo adhimu.
Wakipata chakula.
wakiyarudi magoma kusherehekea Muungano.
Mdau wako wa nguvu akifurahia siku hii adhimu.
Baadhi wageni waalikwa.CHANZO MTAA KWA MTAA BLOG
No comments:
Post a Comment