Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 4, 2014

TAZAMA PICHA ZA KAMPENI SAFISHA JIJI,WAFANYABIASHARA WALIA NA MANISPAA

001 (4)Tuache tunasoma bwana wewe!: Wananchi wakimuangalia mgambo wa Manispaa ya Ilala wakati akichukua magazeti katika moja ya meza maeneo ya Posta mpya jijini Dar es Salaam leo.Mkoa wa Dar es Salaam upo katika operesheni kabambe ya kusafisha jiji kwa kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara ndogo ndogo maeneo yasioruhusiwa wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
003 (4) Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti.004 (4)Mgambo wakiondoa kibanda cha Kampuni ya Simu ya Tigo.
005 (3)Ooh! Hamtaki kuondoka?: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.

006 (3)Hapa ni Eneo la Posta Mpya .
Katika hatua nyingine, nao wafanyabiashara wadogo wadogo stendi ya mabasi ya abiria ya Mwenge wamekumbwa na kadhia hiyo kama inavyoonekana katika picha za chini
0008Kweli jamani?: Wafanya biashara wa Stendi ya Daladala Mwenge jijini Dar es Salaam wakiwa hawana lakufanya wakati  zoezi la bomoa bomoa likiendelea
0009Thubutu kuleta fujo:  Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.00010Hili nalo si mahala pake: Mgambo akiondoa moja ya toroli eneo la Mwenge.00011Usilete mchezo: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa kwenye doria.00012Lazima utulie:  Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwadhibiti wafanya biashara eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI

No comments:

Post a Comment