skip to main |
skip to sidebar
Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!
Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl.
Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua
pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa
sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na
suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge
Maalum.
Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu
na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu
Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale
aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, “Iwapo umma wa Zanzibar bila
ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa
Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu
kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo
washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la
kihistoria kama Muungano'.
Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe
akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema
mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa
kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.
Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya
kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania,
Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa
Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu
Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.
Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu
safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl.
Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.
Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere
alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya
Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi
na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa
serikali mbili).
Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba
wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa
anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.
Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo
hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.
Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe
wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke
mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha
waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli
usijulikane!.
Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.
Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu
watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji
uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za
waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia
mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali
au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza
Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na
wadanganyifu.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.chanzo JF
No comments:
Post a Comment