Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 23, 2014

WASAIDIZI WA MOYES, STEVE ROUND NA JIMMY LUMSDEN NAO WATIMULIWA

David-Moyes
Muda mchache baada ya klabu ya Manchester United kuthibitisha kumtimua kazi kocha David Moyes, shirika la utangazaji wa Uingereza BBC limetangaza kwamba makocha wasaidizi wa Moyes, Steve Round na Jimmy Lumsden nao wameondolewa kwenye vibarua vyao.

Wakati huo huo imethibitishwa kwamba Ryan Giggs na Nicky Butt wataiongoza timu hiyo katika michezo minne iliyobakia.
Hata hivyo mpaka sasa majina ya kocha Uholanzi  Louis Van Gaal, wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp, Atletico Madrid’s manager Diego Simeone na Ryan Giggs wanatajwa kuewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kuanzia msimu ujao.

No comments:

Post a Comment