skip to main |
skip to sidebar
Yanga na Simba zatoka sare ya 1 - 1 Taifa.
Pambano la watani wa jadi limemalizika kwa sare katika mchezo mkali wa
ligi kuu uliofanyika uwanja wa taifa. Simba waliandika bao la kwanza
kupitia kwa Haruna Chanongo katika dakika ya 75 kufuatia kazi nzuri ya
Uhuru Selemani huku Yanga wakisawazisha katika dakika 86 kupitia Simon
Msuva.
Pambano hili lilitawaliwa na vituko ikiwemo Didier
Kavumbagu kupewa kadi ya njano baada ya kulichukua taulo la Ivo Mapunda
na kwenda kulitupa kwa mashabiki na baadae shabiki wa Yanga kuruka uzio
na kulikwapua kwa mara ya pili. Hata hivyo timu zote zilicheza mchezo wa
kuvutia na kukosa nafasi nyingi za wazi.
No comments:
Post a Comment