Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram
Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa
nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya
Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo,
kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika
kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara. Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja
wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake
hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.chanzo BBC
-
*MAENDELEO BANK - PLC, inatarajia kufanya Mkutano mkuu wa 4 wa mwaka
Mkutano huo utakaowakutanisha Wanahisa wote utafanyika Juni 23 mwaka huu
kwenye ukum...
No comments:
Post a Comment