Serikali ya Marekani imewatuma wanajeshi wa ziada nchini Nigeria ili kushirikiana na wanajeshi wa taifa hilo kwa kuwatafuta wasichana zaidi ya 200 waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram.
Kundi hili la Boko Haram linatuhumiwa pia kutekeleza mfululizo wa mashambulizi katika miji mbalimbali hususan kaskazini na hivi karibuni katika mji wa Jos katikati mwa nchi.
Wanajeshi 80 wa Marekani wametumwa nchini Chad ili kuendesha “operesheni ya ujasusi, uchunguzi na ukaguzi katika anga la kaskazini mwa Nigeria na majimbo jirani”, rais Barack Obama amesema jana jioni katika barua aliyotumia bunge la taifa hilo.
Wanajeshi hao watatumia ndege isiyo na rubani ambayo haitokua na silaha yoyote kwa kufanya ukaguzi na upelelezi katika maeneo yoyote yanayoshukiwa kwamba wamefichwa wasichana hao, amesema msemaji wa jeshi, kanali Steve Warren, bila hata hivo ktoa taarifa zaidi kuhusu aina ya ndege hio iliyotumwa.
Idadi hio ya wanajeshi na vifaa, inaongezwa katika idadi nyingine ya wanajeshi vifaa viliyotumwa nchini Nigeria tangu juma liliyopita, ikiwa ni pamoja na ndege zisiyo na rubani, ndege ya ujasusi, na timu nyingi za wataalamu na washauri ambao wanashirikiana na jeshi la Nigeria katika harakati za kuwatafuta wasichana hao.
Familia za watoto hao hazina taarifa yoyote kuhusu wapi walioko watoto zao, tangu walipotekwa nyara na kundi la wanamgambo wa kislamu la Boko Haram Aprili 14 mwaka 2014.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, alitupilia mbali pendekezo liliyotolewa na kiongozi wa kundi la Boko Hara, Abubakar Shekau, la kubadilishana wafuasi wa kundi hilo wanaozuiliwa jela na wasichana hao.
Wakati huo huo Jeshi la Nigeria limeanzisha tangu jumatano wiki hii zoezi la kusajili watu wanotaka kujiunga na jeshi kwa hiyari yao kwa lengo la kupambana na kundi la Boko Haram
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment