Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, May 13, 2014

MBEYA CITY FC YAANGUKIA KUNDI LA KIFO CECAFA NILE BASIN, MWAMBUSI APANGA MAJESHI YAKE


WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc imepangwa kundi B katika michuano mipya ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)  ijulikanayo kwa jina la `CECAFA Nile Basin` inayotarajia kushika kasi kuanzia mei 22 hadi juni 4 mwaka huu nchini Sudan ikijumuisha timu 16.
Katika droo ya michuano hiyo iliyopangwa leo, Mbeya City imepangwa  na timu za AFC Leopards ya Kenya),  El Merreikh Al Fasher ya Sudan na  Elman ya Somalia.
Kundi A: El Merreikh ya Sudan, Victoria University ya Uganda, Malakia ya Sudan Kusini na Polisi ya Zanzibar.
Kundi:  Al Ahli Shandi ya Sudan, Al Masry ya Misri, Defence ya Ethiopia na  Dkhill  ya Djibouti.

No comments:

Post a Comment