Mmoja wa majeruhi akitolewa eneo la tukio.
MLIPUKO
katika mgodi wa makaa ya mawe nchini Uturuki umesababisha vifo vya zaidi
ya wachimbaji migodi 200 na kujeruhi wengine kadhaa.Mlipuko huo umetokea jana katika mji wa Soma mkoa wa Manisa.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa na kifusi chini ya mgodi.
Wakati mlipuko huo ulipotokea, wafanyakazi 580 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia sehemu salama.
No comments:
Post a Comment