Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 16, 2014

Nahodha, baharia 3 washtakiwa kuua Korea

Rais wa Korea Kusini, Park Geune-hye akitoa rambirambi zake kwa mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliokufa maji kwenye feri mwezi uliopita.
Nahodha na wafanyakazi wengine watatu wa feri iliyozama katika ufuo wa Bahari Korea Kusini mwezi uliopita wameshitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Wanashitakiwa kwa kuondoka kwenye feri hiyo, ijulikanayo kama Sewol, huku wakiwambia abiria wao kuwa wasiondoke katika chombo hicho.
Wafanyakazi wengine 11 wa meli hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazini.
Zaidi ya abiria 280 - wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule ya upili karibu na Seoul - walikufa maji wakati feri hiyo ilipozama.ChanzoBBC

No comments:

Post a Comment