Kiongozi
wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amezungumzia janga la mateso dhidi ya
wayahudi wakati wa utawala wa Nazi- maarufu kama Holocaust, wakati wa ziara
yake katika makavazi ya Yad Vashem Holocaust mjini Jerusalem.
Aliweka
shada la maua katika ukumbi huo wa ukumbusho na kusikiza hadithi za manusura wa
janga hilo baya la kihistoria kuwai kuwakumba wayahudi.
Awali
Papa alizuru eneo la kumbukumbu la wayahudi waliouwawa kutokana na mashambulio
ya kigaidi pamoja na kuomba katika maeneo takatifu kwa waisraeli magharibi mwa
ukuta huko Jerusalem.
Papa
anakamilisha ziara yake ya siku tatu mashariki ya kati hii leo kwa kuzuru
msikiti wa zamani wa al-Aqsa na kuwaomba waislamu kuwa na upendo.
Amapokelewa
vyema na waisraeli na wapalestina na hata kuwaalika marais wa nchi hizo katika
Vatican.
Viongozi
hao wawili Shimon Peres wa Israel na Mahmoud Abbas wa Palestina wameelezea
matumani ya kumtemblea Papa.
Akiongea
na mufti wa Jerusale, Ppa alitoa wito kwa wakristo, wayahudi na waisilamu
kupendana.
No comments:
Post a Comment