CHELSEA imethibitisha kuwa mlinda mlango wake namba moja, Petr Cech tayari amefanyiwa upasuaji wa bega lake na sasa anatarajia kurudi uwanjani baada ya wiki 8 au 10.
Kipa huyo raia wa Jamhuri ya Czech aliteguka bega lake katika mchezo wa kwanza wa UEFA dhidi ya Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Calderon na baada ya hapo kocha Jose Mourinho amelazimika kumtumia Mark Schwarzer katika mechi za mwisho za msimu huu.
Hata hivyo, mashabiki wa Chelsea wamepata ahueni baada ya klabu kuthibitisha kuwa kipa huyo amefanikiwa kufanyiwa upasuahi na ataendelea kuimarika wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
Taarifa iliyoandikwa katika mtandao rasmi wa Twita wa Chelsea amesomeka: “Petr Cech amefanikiwa kufanyiwa upasuaji leo (jana) kufuatia kuteguka beki lake. Atakaa nje kwa miezi 8 hadi 10.”
Bado Cech ataendelea kuwa kipa namba moja wa Chelsea msimu ujao, huku Thibaut Courtois akitarajia kurudi katika klabu yake ya Atletico Madrid baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo.
Cech amecheza mechi 46 za mashindano yote msimu huu na amekuwa kipa namba moja tangu alipojiunga na Chelsea kutoka Rennes ya Ufaransa mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment