Nyota wa Chelsea, Luiz yuko njia kuelekea PSG kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 50.
NDANI ya saa 48 zajazo, David Luiz anaweza kujiunga na Paris St Germain kwa dau nono la paundi milioni 50.
Kiwango
halisi cha ada ya uhamisho kitatajwa na klabu, lakini uhamisho wa beki
huyo wa Chelsea mwenye miaka 27 utavunja rekodi ya dunia kwa uhamisho wa
mabeki.
PSG
iliweka rekodi ya kuwasajili mabeki wawili Marquinhos na Thiago Silva
kwa dau nono zaidi, lakini kama watamnasa Luiz kwa mkwanja huo watavunja
rekodi hiyo.
Kama
dau hilo litakubaliwa Stamford Bridge, PSG wataomba ruhusa kwa kocha
wa Brazili Luiz Felipe Scolari ili wakamchukua vipimo vya afya wakati
huu anapojiandaa na kombe la dunia.
PSG
wanaamini kumsajili Luiz watakuwa wamefanikiwa kusajili beki bora zaidi
duniani na usiku wa jana walionekana kuwa tayari kulipa kiwango
chochote watakachohitaji Chelsea.
Matajiri hao wa Ufaransa wanataka kuonesha umwamba wao wa kifedha kwa mara nyingine tena majira ya kiangazi.
Vyanzo
vya habari mjini Paris vimethibitisha kuwa PSG wanajipanga mapema
kuwapiga bao Barcelona na Bayern Munich wenye nia ya kumsajili.
Na inaaminika kuwa kwa dau hilo PSG hawana mpinzani.
Chelsea watatumia fedha hizo kuimarisha kikosi chao kwa kumchukua nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa.
No comments:
Post a Comment