Mwanariadha Usain Bolt hana raha, anatafuta viatu vyake vilivyoibwa.
Mwanariadha huyo bingwa wa Olympic wa mbio fupi
sasa ameeingia kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa twitter ulio na
zaidi ya mashabiki millioni 3 wanaomfuatilia, akisihi 'jamani najua si
tumarafiiki.., aliyeonea viatu vyangu au aliyenavyo tafadhali
uvirudishe'!Majajusi wa Scotland Yard wanasema viliibwa wiki iliyopia mtaa wa Craydon huko London maeneo ya viwandani vilipokuwa vimeekwa kama maonyesho.
Pia nao wanasihi atakaekuwa na fununu yoyote kuvihusu apige ripoti polisi.
Picha za viatu hivyo alivyovaa Usain alipotwaa ushindi zimezagaa mitandaoni, na sasa anaweka saini pair nyengine atakayoipelekea huko Uingereza.
Wadadisi wanasema itabidi ulinzi wa viatu hivyo uimarishwe zaidi.
No comments:
Post a Comment