skip to main |
skip to sidebar
Wadau wa elimu mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wiki ya elimu itakayo fanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Wadau wa elimu mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wiki ya elimu itakayo fanyika kitaifa
mkoani Dodoma.
Akizungumza katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Mkuu wa Mkoa
Wa Dodoma Dr Rehema nchimbi amesema mkoa wa Dodoma ndio
mwenyeji wa sherehe hiyo kutokana na kwamba itazinduliwa Kitaifa Mkoani
hapa katika viwanja vya jamhuri.
Aidha Dr Nchimbi amezitaka taasisi zote za elimu kuweka mabanda katika
viwanja vya jamuhuri ili kuonyesha utendaji kazi wa taasisi hizo.
Pia amekitaka chama cha walimu CWT kuweka banda katika viwanja hivyo
ili watu wakitambue chama hicho na kuwataka walimu kuwa na mshikamano
ili
kufanikisha wiki ya elimu kikamilifu.
Maadhimisho ya wiki ya Elimu yanatarajiwa kuanza tarehe 3Mei mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment