Mahakama moja nchini Israel
imempa kifungo cha miaka sita jela aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel
Ehud Olmert kwa kosa la kupokea hongo.
Bwana Olmert alipatikana na hatia mwezi machi
katika kile kilichojulikana kama 'swala la eneo takatifu' ambapo hongo
ilitolewa ili kuharakisha ujenzi wa majumba ya kifahari mjini Jerusalem.Mashitaka yaliomkabili yalitekelezwa wakati Olmert alipokuwa meya wa mji wa Jerusalem na baadaye akiwa waziri wa serikali.
Ehud Olmert alimrithi Ariel Sharon kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006 baada ya Sharon kuugua ugonjwa wa kiharusi.
Alijiuzulu mnamo mwaka 2008.CHANZO BBBC
No comments:
Post a Comment