Hii ni neema nyingine kwa Diamond Platnumz, baada tu ya kuwa
verifie kwenye mtandao wa twiter, hatimaye sasa kuwa Verified kwenye mtandao wa
kijamii wa Facebook,
hii inamaanisha kuwa kampuni ya Facebook hivi sasa
inamtambua Diamond Platnumz kuwa kama msanii maarufu wa kimataifa, nafasi hii
wanatokea kupata wasanii wachache sana na watu maarufu ambao wanapata bahati ya
kujulikana na makampuni makubwa kama haya. Mwanamitindo wakimataifa Flaviana
Matata ni mmoja wa watu maarufu watokao nchin Tanzania wanaotambuika na kampuni
hiyo, na ni moja ya watu maarufu ambao account yao ipo Verified kama hii ya
Diamond Platnumz. Huu ni mwaka mzuri sana kwa Diamond Platnumz kwa matukio
yanayoendelea kumtokea, na kuzidi kumpa jina kubwa ulimwenguni kupitia muziki
wake huu wa Style yake ya kipekee iliyopewa jina la AfroPop.
No comments:
Post a Comment