Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni usiku wa mwisho kwa kupiga kura za kuwania tuzo za MTM Mama ambapo listi ya washindi ilitajwa na Diamond Platnumz mwimbaji kutoka Tanzania hakuweza kushinda kwenye tuzo hizo.
Mbali na kuto shinda mwimbaji wa Bongo Fleva huyu Diamond Platnumz ametoa shukrani na yake ya moyoni kupitia ukurasa wake wa Instagram kwakuandika hayo hapo chini.
''Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV...Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo... pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema.... Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine...Next stop #BET!!!... Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii''


No comments:
Post a Comment