Ni msiba mzito umeikumba Kambi ya timu ya Taifa ya Ivory
Coast baada ya wachezaj iwake muhimu Kolo na Yaya Toure kupata msiba mkubwa wa
kufiwa na mdogo wao wa damu aitwae Ibrahim Toure, aliyefariki mapema leo kwa
Ugonjwa wa Kansa. Na hivi sasa wachezaji hao wanataraji kurudi kwa Abdijan
kutoka walipo na timu hiyo nchini Brazil kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa
ajili ya taratibu za mazishi ya mdogo huyo aliyefariki jijini Manchester
alipokuwa anakaa kwa kaka yake Yaya ambaye ni kiungo nyota wa Mabingwa wa soka
England Man City. Ibrahim ambaye alikuwa pia ni mwanasoka mahiri katika nafasi
ya ushambuliaji alishawahi kuzichezea club za El Magassah ya Egypt na El Safa
ya Lebanon alikuwa ni mmoja kati ya mastaff wakubwa ndania ya timu ya Man City
kiasi cha kuweza kusafiri na timu kwenye mechi zake kwa umaarufu wa kaka yake
Yaya.
WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS MISRI NA
KUWAKABIDHI BENDERA YA TAIFA.
-
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe....
55 minutes ago


No comments:
Post a Comment