Waimini wa kiisilamu wanaamndamana kupinga wakristo kutumia
neno Allah
Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa
Katholiki nchini humo kumuita Mungu "Allah" katika gazeti lao la
lugha ya ki Malay.
Kesi hiyo ilianza mwaka 2007 pale ambapo serikali ilitishia
kusimamisha huduma za gazeti hilo la kila wiki la kanisa katoliki, The Herald,
ikiwa litaendelea kumuita Mungu, Allah.Walidai kuwa wakristo wanawakanganya
waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa.Uamuzi huo, ni
mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki
zilizochukua muda wa miaka saba na ambao umesababisha mashambulizi katika
makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh katika mwaka wa
2010.Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu, Allah katika
lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda mrefu sana.Mahakama nayo imeshikilia
uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo.
Viongozi wa kanisa wanaogopa kuwa uamuzi huo utasababisha
kizingiti kwa washiriki wake milioni mbili.Mgongano huo kuhusu neno hilo moja
umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofauti tofauti
lilivyogawanyika.Wanaharakati wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje
ya majumba ya koti,wengi wao wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu, Allah,
kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo
wamekana.Mwanasheria mmoja anayewakilisha kanisa katholiki anashauri kuwa bado
wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.Pia kuna wakristo wengine
wanaoleta chochezi za kisheria kama hizo, dhidi ya uamuzi huo wa serikali.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment