Ladha kadhaa za Shisha kpigwa marufuku kwa hofu kuwa zinachanganywa na dawa za kulevya
Shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Kenya,
NACADA, limeharamisha ladha kumi na tisa za Shisha.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu mtendaji wa shirika hilo Fazul
Mohammed, shirika hilo kwa ushirikiano na wanasayansi wa serikali waligundua
kuwa ladha hizo wakati mwingi zinakuwa zimechanganywa na madawa ya kulevya kama
vile Cocaine na Heroine.
Utafiti wao waliufanya kisiri katika mikahawa maarufu yenye
kuuza Shisha na hapo ndipo waligundua kuwa nyingi ya ladha za Shisha huwa
zimechanganywa na madawa ya kulevya.
Baadhi ya ladha hizo pia ziligunduliwa kuwa na Bhangi.
Mwenyekiti wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Kenya,
John Mututho
Akiongea na BBC bwana Fazul alisema kuwa shirika hilo
linatafakari kupiga marufuku Shisha kwa sababu ya madhara yake kwa afya ya
watumiaji na hasa kwa kuwa nyingi zinachanganywa na madawa ya kulevya.Ladha
hizo ambazo zinapaswa kuondoshwa sokoni mara moja ni pamoja na Al Fakher yenye
ladha ya strawberry , Al Fakher yenye ladha ya chungwa , Al Fakher yenye ladha
ya tufaha, Al Fakher vanilla , Al Fakher Mapera, Al Fakher appeals, Al Fakhar
chungwa ikiwa na ladha ya mint na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Bwana Fazul , kwa wale watakoapatikana
wakitumia Shisha lenye ladha hizo ambazo zimepigwa marufuku, watashitakiwa.
Mwenyekiti wa tume ya shirika hilo, John Mututho,
amenukuliwa akisema watakaopatikana wakiuza au kutumia bidhaa hizo,
watafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment