Sehemu ya chumba cha kupumzikia kilichobakiwa na kochi na
zulia.
Ilisemekana kwamba wakati hayo yakiendelea, Mbasha alikuwa
nyuma ya nondo za Mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam ambako alishikiliwa.
Kwa mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana
dhidi ya kesi yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka
17, alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta hakuna
vitu ndani!
Sehemu ya chumba cha kupumzikia kilichobakiwa na kochi na
zulia.
Ilisemekana kwamba wakati hayo yakiendelea, Mbasha alikuwa
nyuma ya nondo za Mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam ambako alishikiliwa.
Kwa mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana
dhidi ya kesi yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka
17, alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta hakuna
vitu ndani!
Chumba kingine kilichosafishwa kabisa bila ya samani yoyote.
Habari zilidai kwamba alipowauliza majirani kama walimuona
mtu akiingia ndani walimwambia mkewe (Flora) ndiye alikuwa akiingia na kutoka
mara kwa mara.Ilielezwa kuwa vitu hivyo vilihamishwa Juni 16 ambapo Mbasha
alitoka mahabusu Juni 17, yaani siku moja tu.
KITANDA CHA BEI MBAYA ::Baadhi ya vitu vilivyodaiwa
kuchukuliwa nyumbani hapo ni kitanda cha bei mbaya walichokuwa wakilalia kwenye
chumba cha baba na mama huku akimwachia neti ikiwa inaning’inia.
SUTI ZA MAREKANI
Vingine ni makochi huku akibakisha sofa ndogo ya mtu mmoja,
vitu vyote jikoni na nguo (suti za bei mbaya, walizonunua wakati wakiwa
Marekani).
Pia alidaiwa kukomba vile vidani vyote vya dhahabu.
Mwandishi wa Global Bw. Harun Sanchawa akipata undani wa
habari kutoka kwa baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, mzee Maneno.
ZAIDI YA MIL. 13
Ukiacha zile hati za nyumba, viwanja na mashamba, gharama ya
vitu vyote vilivyochukuliwa ndani ni zaidi ya Sh. milioni 13 za Kitanzania
(kama zile ambazo Wema Isaac Sepetu alizomlipia Kajala Masanja asiende jela).
AMWAGA CHOZI
Baada ya kukutana na mazingira ya aina hiyo, lilikuwa ni
pigo lingine zito kwa Mbasha ambaye alijikuta akimwaga chozi kwa mara nyingine
kwa sababu ya mkewe Flora aliyedumu naye katika ndoa kwa takriban miaka 12.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha aliumia kupita kiasi huku akiomba
Watanzania waone ubaya aliotendewa.
Bw. Harun Sanchawa akihojiana na mama mzazi wa Emmanuel
Mbasha.
AMANI LAPEKUWA CHUMBA HADI CHUMBA
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Amani lilifika nyumbani
hapo ambapo lilipata mwanya wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kisha kupekuwa
chumba hadi chumba na kujionea kulivyokuwa kweupe huku madirishani mapazia
yakiendelea kubembea kwa upepo mkali uliopo Dar kwa sasa.
Kimuonekano, nyumba hiyo ilikuwa kama kuna familia ilihama
hivyo inahitaji kupangishwa au kuhamiwa na mwingine.
Bw. Emmanuel Mbasha.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha kuzungumzia ishu hiyo alikiri kukuta
hali hiyo nyumbani kwake baada ya kupata dhamana.
“Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta ufunguo wa nyumba kwa
majirani. Niliwauliza kama kulikuwa na mtu anaingia nyumbani nikaambiwa ni
Flora. Kama mnavyoona kuna vitu vingi vya ndani havipo,” alisema Mbasha.
Alipoulizwa kama ana uhakika kuwa mhusika ni Flora, Mbasha
alisema yeye alikuta nyumba nyeupe.
Jitihada za kumpata
Flora hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani haikuwa hewani juzi
Jumanne mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
Flora Mbasha.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya Mbasha kukabiliwa na kesi hiyo ya madai ya ubakaji
wa ndugu wa Flora, Mei 23 na 25, mwaka huu, tayari kulikuwa na mgogoro wa ndoa.
Flora alishaondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza jijini
Dar.
NINI KINAENDELEA?
Wakati kesi ya ubakaji ikiendelea kwenye Mahakama ya Wilaya
ya Ilala, Dar huku Mbasha akiwa nje kwa dhamana, kuna jitihada zinazoendelea
ili warudiane kwani kashfa hiyo inashusha upako wa huduma yao kwa jamii huku
wote wakiwa tayari kwa suluhu.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment