Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 2, 2014

NI VILIO;;;;TAZAMA PICHA JINSI MWILI WA MTOTO ALIYEFICHWA KWENYE BOKSI UKIPOKELEWA MOROGORO KUZIKWA LEO


Jeneza lenye mwili wa marehemu Nasra Rashid likibebwa kuingiza katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ukitokea Dar es Salaam ambako mtoto huyo alilazwa kwa matibabu zaidi kutokana na kuishi katika boksi kwa kipindi cha miaka minne tangu kuzawaliwa kwake. PICHA/MTANDA BLOG.


 
NASRA ENZI ZA UHAI WAKE.

Kutokana na ratiba iliyotolewa na viongozi wa ustawi wa jamii mwili wa Nasra utatarajiwa kuwasiri uwanja wa jamhuri kuanzia majira ya saa 2 asubuhi na wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake watapata fursa ya kuaga kisha saa 5 asubuhi hiyo hiyo msafara utaelekea katika makaburi ya Kolla kwa ajili ya mazishi.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Jole Bendera anatarajia kuwaongoza wananchi kuaga mwili huo.


Mhudumu wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti akiwa amefungua jeneza ili kutoa mwili tayari kwa kuhifadhi katika jokofu.

Mama Mlezi wa Nasra Josephine Joel na Mwandishi wa habari wa gazeti la habarileo Agnes Haule wakiwa kwenye huzuni mara baada ya mwili huo kuhifadhi katika chumba cha maiti.PICHA/MTANDA BLOG

Baba mzazi wa Nasra (aliyeshika shavu) Rashid Mvungi akisikiliza jambo eneo la uwanja wa chumba cha kuhifadhia maiti.

Hapa akionekana mwenye huzuni kutokana na tukio hilo.

Mama Mlezi wa Nasra Josephine Joelakizungumza jambo na waandishi wa habari.

Akiteremka katika gari baada ya msafari uliobeba mwili w

a marehemu mtoto wake Nasra kuwasili eneo hilo. 


Mtoto Nasra Rashid Mvungi (4), aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho za uhai wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje kunichukua”.
Nasra ambaye alikuwa akitibiwa MNH, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya hali yake kubadilika Alhamisi iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kupata hewa ya oksijeni.

Mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa kuzungumza maneno mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada maalumu.

“Sitaki waje kunichukua, sitaki, sitaki, wasije kunichukua, bibi Nasra umesikia,” ni maneno aliyokariri mlezi huyo ambayo yalikuwa yakirudiwarudiwa na Nasra saa chache kabla ya hajawa mahututi na kupelekwa ICU.

Josephine alisema mtoto huyo pia kila mara alikuwa akidai apewe chips na soda na kwamba hadi mauti yalipomkuta alikuwa akitibiwa maradhi ya homa ya mapafu ‘nemonia’.

“Nasra alifariki saa 7.30 usiku, tangu Alhamisi iliyopita hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na imeendelea kuwa hivyo hadi alipofariki dunia,” alisema na kuongeza:

“Bado niko Muhimbili nawasubiri watu wa ustawi wa Jamii kutoka Morogoro wao ndiyo watakuwa na uamuzi kuhusu mazishi ya mtoto huyo,” alisema.

Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Eligaeshi alithibitisha kifo cha mtoto huyo, ambaye alipokewa hospitalini hapo Mei 26 mwaka huu akitokea Morogoro na kwamba hali yake ilibadilika ghafla juzi saa 2:00 usiku.

“Jitihada za madaktari zilifikia kikomo saa 7:30 usiku, baada ya mtoto huyo kupoteza maisha,” alisema.

Kuzikwa kishujaa
Ofisa ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti amsema kuwa mazishi ya Nasra yatatanguliwa na ibada itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho katika Uwanja wa Jamhuri kesho, hatua ambayo alisema inatokana na baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mateso yake.
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment