KIKOSI cha Nigeria kimefanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 inayoendelea nchini Brazil usiku huu.
Nigeria wametinga hatua hiyo wakiwa na pointi 4 mbali na kupoteza mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwa mabao 3-2. Wamefuzu katika kundi F wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Argentina.
Timu nyingine za Afrika ambazo bado zinategemewa na mashabiki ni Algeria kutoka kundi H na Ghana ya kundi G. Timu za Afrika zilizoaga mashindano hayo mpaka sasa ni Cameroon na Ivory Coast.

No comments:
Post a Comment