Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 21, 2014

Simba SC yatangaza iliowatema

 
Henry Joseph


KLABU ya Simba imetangaza rasmi kuachana na nyota wake wanne ambao mikataba yao imefikia tamati na tayari imewaambia watafute maisha sehemu nyingine.
Wachezaji hao waliofungashiwa virago ni Haruna Shamte, Henry Joseph, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ pamoja na Uhuru Seleman lakini kuna wengine ambao wapo mbioni kuachwa.
Hatua hiyo imetokana na klabu hiyo kwa sasa kutokuwa na uhakika wa kufanya usajili katika siku za hivi karibuni kutokana na kutokuwepo kwa viongozi watakaosimamia zoezi hilo, hali iliyoufanya uongozi wa klabu hiyo kufikia hatua hiyo.

Ramadhan Chombo ‘Redondo’


Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba ambaye anamaliza muda hivi karibuni, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wachezaji hao ni bora wakatafute maisha sehemu nyingine kwani wakiendelea kusubiria, mambo yanaweza kwenda ndivyo sivyo.
“Mpaka sasa haijulikani ni lini watapatikana viongozi wapya watakaosimamia zoezi zima la usajili, maana mchakato wa kuwapata viongozi umezongwa na matatizo mengi na juzi tu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza kuusimamisha.
 
Ramadhani Haruna Shamte.


“Watakaoangaliwa zaidi ni wale wenye mikataba kwa sababu hata kama wataachwa, watakuwa na uhakika wa kulipwa, hivyo kwa wale ambao mikataba yao imeisha, ni bora wakatafuta sehemu za kwenda,” alisema Mzee Kinesi na kuongeza:



“Wakati michuano ya ligi kuu msimu uliopita ilipofikia tamati, tulikaa kikao na wachezaji na kuwaambia uongozi wetu ambao unamaliza muda wake hautafanya usajili utakaohusika, jambo hilo litawahusu wale watakaoingia madarakani.

No comments:

Post a Comment